Yoeli 3:18
Joel 3:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Katika siku hiyo milima itadondosha divai mpya, na vilima vitatiririka maziwa; mabonde yote ya Yuda yatatiririka maji. Chemchemi itatiririka kutoka kwenye nyumba ya Bwana na kunywesha Bonde la Shitimu.*
Joel 3:18 in English
Joel 3:18 · Berean Standard Bible
And in that day the mountains will drip with sweet wine, and the hills will flow with milk. All the streams of Judah will run with water, and a spring will flow from the house of the LORD to water the Valley of Acacias.*
Context
16Bwana atanguruma kutoka Sayuni
na mshindo wa ngurumo kutoka Yerusalemu;
dunia na mbingu vitatikisika.
Lakini Bwana atakuwa kimbilio la watu wake,
ngome imara kwa ajili ya watu wa Israeli. 17“Ndipo mtakapojua kwamba Mimi, Bwana Mungu wenu,
nakaa Sayuni, mlima wangu mtakatifu.
Yerusalemu utakuwa mtakatifu;
kamwe wageni hawatavamia tena. 18“Katika siku hiyo milima itadondosha divai mpya,
na vilima vitatiririka maziwa;
mabonde yote ya Yuda yatatiririka maji.
Chemchemi itatiririka kutoka kwenye nyumba ya Bwana
na kunywesha Bonde la Shitimu.* 19Lakini Misri itakuwa ukiwa,
Edomu itakuwa jangwa tupu,
kwa sababu ya jeuri waliofanya kwa watu wa Yuda,
ambao katika nchi yao
walimwaga damu isiyo na hatia. 20Yuda itakaliwa na watu milele
na Yerusalemu itadumu vizazi vyote.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.