Native Bible

Job 9:19 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kama ni suala la nguvu, yeye ni mwenye nguvu! Kama ni suala la haki, ni nani awezaye kumwita mahakamani?

Job 9:19 in English

Job 9:19 · Berean Standard Bible

If it is a matter of strength, He is indeed mighty! If it is a matter of justice, who can summon Him *?

Context

17Yeye angeniangamiza kwa dhoruba na kuongeza majeraha yangu pasipo na sababu. 18Asingeniacha nipumue bali angenifunika kabisa na huzuni kuu. 19Kama ni suala la nguvu, yeye ni mwenye nguvu! Kama ni suala la haki, ni nani awezaye kumwita mahakamani? 20Hata kama sikuwa na hatia, kinywa changu kingenihukumu; kama sikuwa na kosa, kingenitangaza kuwa mwenye hatia. 21“Ingawa mimi sina kosa, haileti tofauti katika nafsi yangu; nauchukia uhai wangu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.