Native Bible

Job 9:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Anapopita karibu nami, siwezi kumwona; apitapo mbele yangu, simtambui.

Job 9:11 in English

Job 9:11 · Berean Standard Bible

Were He to pass by me, I would not see Him; were He to move, I would not recognize Him.

Context

9Yeye ndiye Muumba wa nyota za Dubu,* na Orioni,* Kilimia,* na makundi ya nyota za kusini. 10Hutenda maajabu yasiyopimika, miujiza isiyoweza kuhesabiwa. 11Anapopita karibu nami, siwezi kumwona; apitapo mbele yangu, simtambui. 12Anapochukua kwa ghafula, ni nani awezaye kumzuia? Ni nani awezaye kumwambia, ‘Unafanya nini?’ 13Mungu hataizuia hasira yake; hata jeshi kubwa la Rahabu* lenye nguvu linajikunyata miguuni pake.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.