Native Bible

Job 41:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Pumzi yake huwasha makaa ya mawe, nayo miali ya moto huruka kutoka kinywani mwake.

Job 41:21 in English

Job 41:21 · Berean Standard Bible

His breath sets coals ablaze, and flames pour from his mouth.

Context

19Mienge iwakayo humiminika kutoka kinywani mwake; cheche za moto huruka nje. 20Moshi hufuka kutoka puani mwake, kama kutoka kwenye chungu kinachotokota kwa moto wa matete. 21Pumzi yake huwasha makaa ya mawe, nayo miali ya moto huruka kutoka kinywani mwake. 22Nguvu hukaa katika shingo yake; utisho hutangulia mbele yake. 23Mikunjo ya nyama yake imeshikamana imara pamoja; iko imara na haiwezi kuondolewa.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.