Native Bible

Job 39:27 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Je, tai hupaa juu kwa amri yako na kujenga kiota chake mahali pa juu?

Job 39:27 in English

Job 39:27 · Berean Standard Bible

Does the eagle soar at your command and make his nest on high?

Context

25Asikiapo sauti ya baragumu yeye hulia, ‘Aha!’ Hunusa harufu ya vita toka mbali, sauti ya mtoa amri na ukelele wa vita. 26“Je, mwewe huruka kwa hekima yako na kuyakunjua mabawa yake kuelekea kusini? 27Je, tai hupaa juu kwa amri yako na kujenga kiota chake mahali pa juu? 28Huishi juu ya miamba mirefu na kukaa huko usiku; majabali yenye ncha kali ndiyo ngome yake. 29Kutoka huko hutafuta chakula chake; macho yake hukiona kutoka mbali.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.