Native Bible

Job 36:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Wanakufa wangali vijana, miongoni mwa wanaume hanithi wa mahali pa kuabudia miungu.

Job 36:14 in English

Job 36:14 · Berean Standard Bible

They die in their youth, among the male shrine prostitutes.

Context

12Lakini wasiposikiliza, wataangamia kwa upanga, nao watakufa pasipo maarifa. 13“Wasiomcha Mungu moyoni mwao huficha chuki; hata anapowafunga, hawamwombi msaada. 14Wanakufa wangali vijana, miongoni mwa wanaume hanithi wa mahali pa kuabudia miungu. 15Bali wao wanaoteseka huwaokoa katika mateso yao, na kuzungumza nao katika dhiki zao. 16“Yeye anakubembeleza utoke katika mataya ya dhiki, ili kukuweka mahali palipo na nafasi mbali na kizuizi, hadi kwenye meza yako ya faraja iliyojaa vyakula vizuri.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.