Native Bible

Job 30:27 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kusukwasukwa ndani yangu kamwe hakutulii; siku za mateso zinanikabili.

Job 30:27 in English

Job 30:27 · Berean Standard Bible

I am churning within and cannot rest; days of affliction confront me.

Context

25Je, sikulia kwa ajili ya wale waliokuwa katika taabu? Je, nafsi yangu haikusononeka kwa ajili ya maskini? 26Lakini nilipotazamia mema, mabaya yalinijia; nilipotafuta nuru, ndipo giza lilipokuja. 27Kusukwasukwa ndani yangu kamwe hakutulii; siku za mateso zinanikabili. 28Ninazunguka nikiwa nimeungua, lakini si kwa jua; ninasimama katika kusanyiko nikiomba msaada. 29Nimekuwa ndugu wa mbweha, rafiki wa mabundi.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.