Native Bible

Job 30:26 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Lakini nilipotazamia mema, mabaya yalinijia; nilipotafuta nuru, ndipo giza lilipokuja.

Job 30:26 in English

Job 30:26 · Berean Standard Bible

But when I hoped for good, evil came; when I looked for light, darkness fell.

Context

24“Hakika hakuna yeyote amshambuliaye mhitaji, anapoomba msaada katika shida yake. 25Je, sikulia kwa ajili ya wale waliokuwa katika taabu? Je, nafsi yangu haikusononeka kwa ajili ya maskini? 26Lakini nilipotazamia mema, mabaya yalinijia; nilipotafuta nuru, ndipo giza lilipokuja. 27Kusukwasukwa ndani yangu kamwe hakutulii; siku za mateso zinanikabili. 28Ninazunguka nikiwa nimeungua, lakini si kwa jua; ninasimama katika kusanyiko nikiomba msaada.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.