Native Bible

Job 29:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Natamani siku zile nilizokuwa katika ustawi wangu, wakati urafiki wa Mungu wa ndani ulipoibariki nyumba yangu,

Job 29:4 in English

Job 29:4 · Berean Standard Bible

when I was in my prime,* when the friendship of God rested on my tent,

Context

2“Tazama jinsi ninavyoitamani miezi iliyopita, zile siku ambazo Mungu alikuwa akinilinda, 3wakati taa yake iliniangazia kichwani changu, na kwa mwanga wake Mungu nikapita katikati ya giza! 4Natamani siku zile nilizokuwa katika ustawi wangu, wakati urafiki wa Mungu wa ndani ulipoibariki nyumba yangu, 5wakati Mwenyezi alikuwa pamoja nami, nao watoto wangu walikuwa wamenizunguka, 6wakati njia yangu ilikuwa imenyweshewa siagi, nao mwamba ukanimiminia vijito vya mafuta ya zeituni.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.