Native Bible

Job 24:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Hutota kwa mvua za mlimani, nao huikumbatia miamba kwa ajili ya kukosa pa kujisitiri.

Job 24:8 in English

Job 24:8 · Berean Standard Bible

Drenched by mountain rains, they huddle against the rocks for want of shelter.

Context

6Hukusanya chakula mashambani na kuokota masazo katika mashamba ya mizabibu ya waovu. 7Kwa kukosa nguo, usiku kucha hukaa uchi; hawana chochote cha kujifunika baridi. 8Hutota kwa mvua za mlimani, nao huikumbatia miamba kwa ajili ya kukosa pa kujisitiri. 9Mtoto yatima hupokonywa matitini; mtoto wachanga wa maskini hunyakuliwa kwa ajili ya deni. 10Kwa kukosa nguo, hutembea uchi; hubeba miganda ya ngano, lakini huwa na njaa.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.