Native Bible

Job 24:23 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Aweza akawaacha wakapumzika wakijihisi salama, lakini macho yake yanaona njia zao.

Job 24:23 in English

Job 24:23 · Berean Standard Bible

He gives them a sense of security, but His eyes are on their ways.

Context

21Huwafanya mawindo wanawake tasa na wasio na watoto, nao hawaonyeshi huruma kwa wajane. 22Lakini Mungu huwakokota wenye nguvu kwa uwezo wake; ingawa wamestawi, hawana hakika ya maisha. 23Aweza akawaacha wakapumzika wakijihisi salama, lakini macho yake yanaona njia zao. 24Kwa kitambo kidogo hutukuka, hatimaye hutoweka; hushushwa na kukusanywa kama wengine wote, hukatwa kama masuke ya nafaka. 25“Kama hili sivyo, ni nani awezaye kunithibitisha kuwa mwongo, na kuyafanya maneno yangu kuwa si kitu?”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.