Native Bible

Job 20:23 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Atakapokuwa amelijaza tumbo lake, Mungu ataionyesha ghadhabu kali dhidi yake, na kumnyeshea mapigo juu yake.

Job 20:23 in English

Job 20:23 · Berean Standard Bible

When he has filled his stomach, God will vent His fury upon him, raining it down on him as he eats.

Context

21Hakuna chochote kitakachosalia kwa ajili yake ili ale; kufanikiwa kwake hakutadumu. 22Katikati ya wingi wa ustawi wake, dhiki itampata; taabu itamjia kwa nguvu zote. 23Atakapokuwa amelijaza tumbo lake, Mungu ataionyesha ghadhabu kali dhidi yake, na kumnyeshea mapigo juu yake. 24Ijapokuwa aikimbia silaha ya chuma, mshale wa shaba utamchoma. 25Atauchomoa katika mgongo wake, ncha ingʼaayo kutoka ini lake. Vitisho vitakuja juu yake;

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.