Ayubu 1:20
Job 1:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ndipo Ayubu akasimama, akararua joho lake na kunyoa nywele zake. Kisha akaanguka chini katika kuabudu
Job 1:20 in English
Job 1:20 · Berean Standard Bible
Then Job stood up, tore his robe, and shaved his head. He fell to the ground and worshiped,
Context
18Alipokuwa bado ananena, mjumbe mwingine akaja na kusema, “Wana wako na binti zako walipokuwa wakifanya karamu, wakila na kunywa divai katika nyumba ya ndugu yao mkubwa, 19ghafula upepo wenye nguvu ukavuma kutoka jangwani, nao ukaipiga nyumba hiyo pembe zake nne. Ikawaangukia hao watoto nao wamekufa, nami ndimi peke yangu niliyenusurika kukuletea habari!” 20Ndipo Ayubu akasimama, akararua joho lake na kunyoa nywele zake. Kisha akaanguka chini katika kuabudu 21na kusema:
“Nilitoka tumboni mwa mama yangu uchi,
nami nitaondoka uchi,*
Bwana alinipa, naye Bwana ameviondoa,
jina la Bwana litukuzwe.” 22Katika mambo haya yote, Ayubu hakutenda dhambi kwa kumlaumu Mungu kwa kufanya ubaya.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.