Native Bible

John 2:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Mama yake akawaambia wale watumishi, “Lolote atakalowaambia, fanyeni.”

John 2:5 in English

John 2:5 · Berean Standard Bible

His mother said to the servants, “Do whatever He tells you.”

Context

3Divai ilipokwisha, mama yake Yesu akamwambia, “Wameishiwa na divai.” 4Yesu akamwambia, “Mwanamke, nina nini nawe? Saa yangu haijawadia.” 5Mama yake akawaambia wale watumishi, “Lolote atakalowaambia, fanyeni.” 6Basi ilikuwepo mitungi sita ya kuhifadhia maji iliyotengenezwa kwa mawe kwa ajili ya kujitakasa kwa desturi ya Kiyahudi; kila mtungi ungeweza kuchukua vipipa viwili au vitatu.* 7Yesu akawaambia wale watumishi, “Ijazeni hiyo mitungi maji.” Nao wakaijaza ile mitungi mpaka juu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.