Yohana 2:6
John 2:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Basi ilikuwepo mitungi sita ya kuhifadhia maji iliyotengenezwa kwa mawe kwa ajili ya kujitakasa kwa desturi ya Kiyahudi; kila mtungi ungeweza kuchukua vipipa viwili au vitatu.*
John 2:6 in English
John 2:6 · Berean Standard Bible
Now six stone water jars had been set there for the Jewish rites of purification. Each could hold from twenty to thirty gallons.*
Context
4Yesu akamwambia, “Mwanamke, nina nini nawe? Saa yangu haijawadia.” 5Mama yake akawaambia wale watumishi, “Lolote atakalowaambia, fanyeni.” 6Basi ilikuwepo mitungi sita ya kuhifadhia maji iliyotengenezwa kwa mawe kwa ajili ya kujitakasa kwa desturi ya Kiyahudi; kila mtungi ungeweza kuchukua vipipa viwili au vitatu.* 7Yesu akawaambia wale watumishi, “Ijazeni hiyo mitungi maji.” Nao wakaijaza ile mitungi mpaka juu. 8Kisha akawaambia, “Sasa choteni hayo maji kidogo, mpelekeeni mkuu wa meza.”
Hivyo wakachota, wakampelekea.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.