Native Bible

John 12:42 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Lakini wengi miongoni mwa viongozi wa Wayahudi walimwamini, lakini kwa sababu ya Mafarisayo hawakukiri waziwazi kwa maana waliogopa kufukuzwa katika masinagogi.

John 12:42 in English

John 12:42 · Berean Standard Bible

Nevertheless, many of the leaders believed in Him; but because of the Pharisees they did not confess Him, for fear that they would be put out of the synagogue.

Context

40“Amewafanya vipofu, na kuifanya mioyo yao kuwa migumu, ili wasiweze kuona kwa macho yao, wala kuelewa kwa mioyo yao, wasije wakageuka nami nikawaponya.” 41Isaya alisema haya alipoona utukufu wa Yesu na kunena habari zake. 42Lakini wengi miongoni mwa viongozi wa Wayahudi walimwamini, lakini kwa sababu ya Mafarisayo hawakukiri waziwazi kwa maana waliogopa kufukuzwa katika masinagogi. 43Wao walipenda sifa za wanadamu kuliko sifa zitokazo kwa Mungu. 44Yesu akapaza sauti akasema, “Yeyote aniaminiye, haniamini mimi peke yangu, bali yeye aliyenituma.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.