Native Bible

Jeremiah 50:43 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Mfalme wa Babeli amesikia habari kuwahusu, nayo mikono yake imelegea. Uchungu umemshika, maumivu kama ya mwanamke katika utungu wa kuzaa.

Jeremiah 50:43 in English

Jeremiah 50:43 · Berean Standard Bible

The king of Babylon has heard the report, and his hands hang limp. Anguish has gripped him, pain like that of a woman in labor.

Context

41“Tazama! Jeshi linakuja kutoka kaskazini; taifa kubwa na wafalme wengi wanaamshwa kutoka miisho ya dunia. 42Wamejifunga pinde na mikuki; ni wakatili na wasio na huruma. Wanatoa sauti kama bahari inayonguruma wanapoendesha farasi zao; wanakuja kama watu waliojipanga tayari kwa vita ili kukushambulia, ee Binti Babeli. 43Mfalme wa Babeli amesikia habari kuwahusu, nayo mikono yake imelegea. Uchungu umemshika, maumivu kama ya mwanamke katika utungu wa kuzaa. 44Kama simba anayepanda kutoka vichaka vya Yordani kuja kwenye nchi ya malisho mengi, ndivyo nitamfukuza Babeli kutoka nchi yake ghafula. Ni nani aliye mteule, nitakayemweka kwa ajili ya jambo hili? Ni nani aliye kama mimi, na ni nani awezaye kunipinga? Tena ni mchungaji yupi awezaye kusimama kinyume nami?” 45Kwa hiyo, sikia kile Bwana alichokipanga dhidi ya Babeli, kile alichokusudia dhidi ya nchi ya Wakaldayo: Aliye mchanga katika kundi ataburutwa mbali. Yeye ataharibu kabisa malisho yao kwa sababu yao.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.