Yeremia 50:45
Jeremiah 50:45 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa hiyo, sikia kile Bwana alichokipanga dhidi ya Babeli, kile alichokusudia dhidi ya nchi ya Wakaldayo: Aliye mchanga katika kundi ataburutwa mbali. Yeye ataharibu kabisa malisho yao kwa sababu yao.
Jeremiah 50:45 in English
Jeremiah 50:45 · Berean Standard Bible
Therefore hear the plans that the LORD has drawn up against Babylon and the strategies He has devised against the land of the Chaldeans: Surely the little ones of the flock will be dragged away; certainly their pasture will be made desolate because of them.
Context
43Mfalme wa Babeli amesikia habari kuwahusu,
nayo mikono yake imelegea.
Uchungu umemshika,
maumivu kama ya mwanamke katika utungu wa kuzaa. 44Kama simba anayepanda kutoka vichaka vya Yordani
kuja kwenye nchi ya malisho mengi,
ndivyo nitamfukuza Babeli kutoka nchi yake ghafula.
Ni nani aliye mteule,
nitakayemweka kwa ajili ya jambo hili?
Ni nani aliye kama mimi,
na ni nani awezaye kunipinga?
Tena ni mchungaji yupi
awezaye kusimama kinyume nami?” 45Kwa hiyo, sikia kile Bwana alichokipanga dhidi ya Babeli,
kile alichokusudia dhidi ya nchi ya Wakaldayo:
Aliye mchanga katika kundi ataburutwa mbali.
Yeye ataharibu kabisa malisho yao kwa sababu yao. 46Kwa sauti ya kutekwa kwa Babeli, dunia itatetemeka;
kilio chake kitasikika pote miongoni mwa mataifa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.