Yeremia 50:41
Jeremiah 50:41 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Tazama! Jeshi linakuja kutoka kaskazini; taifa kubwa na wafalme wengi wanaamshwa kutoka miisho ya dunia.
Jeremiah 50:41 in English
Jeremiah 50:41 · Berean Standard Bible
Behold, an army is coming from the north; a great nation and many kings are stirred up from the ends of the earth.
Context
39“Kwa hiyo, viumbe vya jangwani na fisi wataishi humo,
nao bundi watakaa humo.
Kamwe haitakaliwa tena
wala watu hawataishi humo kutoka kizazi hadi kizazi. 40Kama vile Mungu alivyoangamiza Sodoma na Gomora
pamoja na miji iliyokuwa jirani nayo,”
asema Bwana,
“vivyo hivyo hakuna mtu yeyote
atakayeishi humo.
Naam, hakuna mtu yeyote
atakayekaa humo. 41“Tazama! Jeshi linakuja kutoka kaskazini;
taifa kubwa na wafalme wengi
wanaamshwa kutoka miisho ya dunia. 42Wamejifunga pinde na mikuki;
ni wakatili na wasio na huruma.
Wanatoa sauti kama bahari inayonguruma
wanapoendesha farasi zao;
wanakuja kama watu waliojipanga tayari kwa vita
ili kukushambulia, ee Binti Babeli. 43Mfalme wa Babeli amesikia habari kuwahusu,
nayo mikono yake imelegea.
Uchungu umemshika,
maumivu kama ya mwanamke katika utungu wa kuzaa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.