Native Bible

Jeremiah 50:39 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Kwa hiyo, viumbe vya jangwani na fisi wataishi humo, nao bundi watakaa humo. Kamwe haitakaliwa tena wala watu hawataishi humo kutoka kizazi hadi kizazi.

Jeremiah 50:39 in English

Jeremiah 50:39 · Berean Standard Bible

So the desert creatures and hyenas will live there and ostriches * will dwell there. It will never again be inhabited or lived in from generation to generation.

Context

37Upanga dhidi ya farasi na magari yake ya vita pamoja na askari wake wote wa kigeni katika safu zake! Wao watakuwa kama wanawake. Upanga dhidi ya hazina zake! Hizo zitatekwa nyara. 38Ukame juu ya maji yake! Nayo yatakauka. Kwa kuwa ni nchi ya sanamu, wao wanaenda wazimu kwa ajili ya sanamu. 39“Kwa hiyo, viumbe vya jangwani na fisi wataishi humo, nao bundi watakaa humo. Kamwe haitakaliwa tena wala watu hawataishi humo kutoka kizazi hadi kizazi. 40Kama vile Mungu alivyoangamiza Sodoma na Gomora pamoja na miji iliyokuwa jirani nayo,” asema Bwana, “vivyo hivyo hakuna mtu yeyote atakayeishi humo. Naam, hakuna mtu yeyote atakayekaa humo. 41“Tazama! Jeshi linakuja kutoka kaskazini; taifa kubwa na wafalme wengi wanaamshwa kutoka miisho ya dunia.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.