Yeremia 50:30
Jeremiah 50:30 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa hiyo, vijana wake wanaume wataanguka barabarani; askari wake wote watanyamazishwa siku ile,” asema Bwana.
Jeremiah 50:30 in English
Jeremiah 50:30 · Berean Standard Bible
Therefore, her young men will fall in the streets, and all her warriors will be silenced in that day,” declares the LORD.
Context
28Wasikilizeni watoro na wakimbizi kutoka Babeli
wakitangaza katika Sayuni
jinsi Bwana, Mungu wetu alivyolipiza kisasi,
kisasi kwa ajili ya Hekalu lake. 29“Waiteni wapiga mishale dhidi ya Babeli,
wote wale wavutao upinde.
Pigeni kambi kumzunguka kabisa,
asitoroke mtu yeyote.
Mlipizeni kwa matendo yake;
mtendeeni kama alivyotenda.
Kwa kuwa alimdharau Bwana,
yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli. 30Kwa hiyo, vijana wake wanaume wataanguka barabarani;
askari wake wote watanyamazishwa siku ile,”
asema Bwana. 31“Tazama, niko kinyume nawe, ewe mwenye majivuno,”
asema Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote,
“kwa kuwa siku yako imewadia,
yaani, wakati wako wa kuadhibiwa. 32Mwenye majivuno atajikwaa na kuanguka,
wala hakuna yeyote atakayemuinua;
nitawasha moto katika miji yake,
utakaowateketeza wote wanaomzunguka.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.