Yeremia 50:32
Jeremiah 50:32 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mwenye majivuno atajikwaa na kuanguka, wala hakuna yeyote atakayemuinua; nitawasha moto katika miji yake, utakaowateketeza wote wanaomzunguka.”
Jeremiah 50:32 in English
Jeremiah 50:32 · Berean Standard Bible
The arrogant one will stumble and fall with no one to pick him up. And I will kindle a fire in his cities to consume all those around him.”
Context
30Kwa hiyo, vijana wake wanaume wataanguka barabarani;
askari wake wote watanyamazishwa siku ile,”
asema Bwana. 31“Tazama, niko kinyume nawe, ewe mwenye majivuno,”
asema Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote,
“kwa kuwa siku yako imewadia,
yaani, wakati wako wa kuadhibiwa. 32Mwenye majivuno atajikwaa na kuanguka,
wala hakuna yeyote atakayemuinua;
nitawasha moto katika miji yake,
utakaowateketeza wote wanaomzunguka.” 33Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote:
“Watu wa Israeli wameonewa,
nao watu wa Yuda pia.
Wote waliowateka wamewashikilia sana,
wanakataa kuwaachia waende. 34Lakini Mkombozi wao ana nguvu;
Bwana Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake.
Atatetea kwa nguvu shauri lao
ili alete raha katika nchi yao,
lakini ataleta msukosuko
kwa wale waishio Babeli.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.