Native Bible

Jeremiah 50:33 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote: “Watu wa Israeli wameonewa, nao watu wa Yuda pia. Wote waliowateka wamewashikilia sana, wanakataa kuwaachia waende.

Jeremiah 50:33 in English

Jeremiah 50:33 · Berean Standard Bible

This is what the LORD of Hosts says: “The sons of Israel are oppressed, and the sons of Judah as well. All their captors hold them fast, refusing to release them.

Context

31“Tazama, niko kinyume nawe, ewe mwenye majivuno,” asema Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, “kwa kuwa siku yako imewadia, yaani, wakati wako wa kuadhibiwa. 32Mwenye majivuno atajikwaa na kuanguka, wala hakuna yeyote atakayemuinua; nitawasha moto katika miji yake, utakaowateketeza wote wanaomzunguka.” 33Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote: “Watu wa Israeli wameonewa, nao watu wa Yuda pia. Wote waliowateka wamewashikilia sana, wanakataa kuwaachia waende. 34Lakini Mkombozi wao ana nguvu; Bwana Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake. Atatetea kwa nguvu shauri lao ili alete raha katika nchi yao, lakini ataleta msukosuko kwa wale waishio Babeli. 35“Upanga dhidi ya Wakaldayo!” asema Bwana, “dhidi ya wale waishio Babeli na dhidi ya maafisa wake na watu wenye busara!

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.