Yeremia 50:14
Jeremiah 50:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Shikeni nafasi zenu kuzunguka Babeli, enyi nyote mvutao upinde. Mpigeni! Msibakize mshale wowote, kwa kuwa ametenda dhambi dhidi ya Bwana.
Jeremiah 50:14 in English
Jeremiah 50:14 · Berean Standard Bible
Line up in formation around Babylon, all you who draw the bow! Shoot at her! Spare no arrows! For she has sinned against the LORD.
Context
12mama yako ataaibika mno,
yeye aliyekuzaa atatahayari.
Atakuwa mdogo kuliko mataifa mengine yote,
atakuwa nyika, nchi kame na jangwa. 13Kwa sababu ya hasira ya Bwana hatakaliwa na mtu,
lakini ataachwa ukiwa kabisa.
Wote watakaopita Babeli watatiwa hofu na kudhihaki
kwa sababu ya majeraha yake yote. 14“Shikeni nafasi zenu kuzunguka Babeli,
enyi nyote mvutao upinde.
Mpigeni! Msibakize mshale wowote,
kwa kuwa ametenda dhambi dhidi ya Bwana. 15Piga kelele dhidi yake kila upande!
Anajisalimisha, minara yake inaanguka,
kuta zake zimebomoka.
Kwa kuwa hiki ni kisasi cha Bwana,
mlipizeni kisasi;
mtendeeni kama alivyowatendea wengine. 16Katilieni mbali mpanzi kutoka Babeli,
pamoja na mvunaji na mundu wake akivuna.
Kwa sababu ya upanga wa mdhalimu
kila mmoja na arejee kwa watu wake mwenyewe,
kila mmoja na akimbilie
kwenye nchi yake mwenyewe.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.