Native Bible

Jeremiah 50:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Katilieni mbali mpanzi kutoka Babeli, pamoja na mvunaji na mundu wake akivuna. Kwa sababu ya upanga wa mdhalimu kila mmoja na arejee kwa watu wake mwenyewe, kila mmoja na akimbilie kwenye nchi yake mwenyewe.

Jeremiah 50:16 in English

Jeremiah 50:16 · Berean Standard Bible

Cut off the sower from Babylon, and the one who wields the sickle at harvest time. In the face of the oppressor’s sword, each will turn to his own people, each will flee to his own land.

Context

14“Shikeni nafasi zenu kuzunguka Babeli, enyi nyote mvutao upinde. Mpigeni! Msibakize mshale wowote, kwa kuwa ametenda dhambi dhidi ya Bwana. 15Piga kelele dhidi yake kila upande! Anajisalimisha, minara yake inaanguka, kuta zake zimebomoka. Kwa kuwa hiki ni kisasi cha Bwana, mlipizeni kisasi; mtendeeni kama alivyowatendea wengine. 16Katilieni mbali mpanzi kutoka Babeli, pamoja na mvunaji na mundu wake akivuna. Kwa sababu ya upanga wa mdhalimu kila mmoja na arejee kwa watu wake mwenyewe, kila mmoja na akimbilie kwenye nchi yake mwenyewe. 17“Israeli ni kundi lililotawanyika ambalo simba wamelifukuzia mbali. Wa kwanza kumla alikuwa mfalme wa Ashuru, wa mwisho kuponda mifupa yake alikuwa Nebukadneza mfalme wa Babeli.” 18Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: “Nitamwadhibu mfalme wa Babeli na nchi yake kama nilivyomwadhibu mfalme wa Ashuru.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.