Yeremia 49:10
Jeremiah 49:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini nitamvua Esau nguo abaki uchi, nitayafunua maficho yake, ili asiweze kujificha. Watoto wake, jamaa na majirani wataangamia, naye hatakuwepo tena.
Jeremiah 49:10 in English
Jeremiah 49:10 · Berean Standard Bible
But I will strip Esau bare; I will uncover his hiding places, and he will be unable to conceal himself. His descendants will be destroyed along with his relatives and neighbors, and he will be no more.
Context
8Geuka na ukimbie, jifiche katika mapango marefu kabisa,
wewe uishiye Dedani,
kwa kuwa nitaleta maafa juu ya Esau
wakati nitakapomwadhibu. 9Je, kama wachuma zabibu wangekuja kwako,
wasingebakiza zabibu chache?
Kama wezi wangekujia usiku,
je, si wangeiba tu kiasi ambacho wangehitaji? 10Lakini nitamvua Esau nguo abaki uchi,
nitayafunua maficho yake,
ili asiweze kujificha.
Watoto wake, jamaa na majirani wataangamia,
naye hatakuwepo tena. 11Waache yatima wako; nitayalinda maisha yao.
Wajane wako pia
wanaweza kunitumaini mimi.” 12Hili ndilo asemalo Bwana: “Kama wale wasiostahili kukinywea kikombe ni lazima wakinywe, kwa nini wewe usiadhibiwe? Hutakwepa kuadhibiwa, ni lazima ukinywe.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.