Yeremia 49:12
Jeremiah 49:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hili ndilo asemalo Bwana: “Kama wale wasiostahili kukinywea kikombe ni lazima wakinywe, kwa nini wewe usiadhibiwe? Hutakwepa kuadhibiwa, ni lazima ukinywe.
Jeremiah 49:12 in English
Jeremiah 49:12 · Berean Standard Bible
For this is what the LORD says: “If those who do not deserve to drink the cup must drink it, can you possibly remain unpunished? You will not go unpunished, for you must drink it too.
Context
10Lakini nitamvua Esau nguo abaki uchi,
nitayafunua maficho yake,
ili asiweze kujificha.
Watoto wake, jamaa na majirani wataangamia,
naye hatakuwepo tena. 11Waache yatima wako; nitayalinda maisha yao.
Wajane wako pia
wanaweza kunitumaini mimi.” 12Hili ndilo asemalo Bwana: “Kama wale wasiostahili kukinywea kikombe ni lazima wakinywe, kwa nini wewe usiadhibiwe? Hutakwepa kuadhibiwa, ni lazima ukinywe. 13Ninaapa kwa nafsi yangu,” asema Bwana, “kwamba Bosra utakuwa magofu na kitu cha kutisha, cha aibu na cha kulaania; miji yake yote itakuwa magofu milele.” 14Nimesikia ujumbe kutoka kwa Bwana:
Mjumbe alitumwa kwa mataifa kusema,
“Jikusanyeni ili kuushambulia!
Inukeni kwa ajili ya vita!”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.