Native Bible

Jeremiah 48:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kwa kuwa mmetumainia matendo yenu na mali zenu, ninyi pia mtachukuliwa mateka, naye Kemoshi* atakwenda uhamishoni, pamoja na makuhani wake na maafisa wake.

Jeremiah 48:7 in English

Jeremiah 48:7 · Berean Standard Bible

Because you trust in your works and treasures, you too will be captured, and Chemosh will go into exile with his priests and officials.

Context

5Wanapanda kwenda njia ya kuelekea Luhithi, wakilia kwa uchungu wanapotembea, kwenye njia inayoshuka kwenda Horonaimu, kilio cha uchungu kwa ajili ya uharibifu kinasikika. 6Kimbieni! Okoeni maisha yenu, kuweni kama kichaka jangwani. 7Kwa kuwa mmetumainia matendo yenu na mali zenu, ninyi pia mtachukuliwa mateka, naye Kemoshi* atakwenda uhamishoni, pamoja na makuhani wake na maafisa wake. 8Mharabu atakuja dhidi ya kila mji, wala hakuna mji utakaookoka. Bonde litaangamizwa na uwanda utaharibiwa, kwa sababu Bwana amesema. 9Wekeni chumvi kwa ajili ya Moabu, kwa kuwa ataangamizwa; miji yake itakuwa ukiwa, pasipo kuwa na mtu atakayeishi ndani yake.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.