Yeremia 48:31
Jeremiah 48:31 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa hiyo namlilia Moabu, kwa ajili ya Moabu yote ninalia, ninaomboleza kwa ajili ya watu wa Kir-Haresethi.
Jeremiah 48:31 in English
Jeremiah 48:31 · Berean Standard Bible
Therefore I will wail for Moab; I will cry out for all of Moab; I will moan for the men of Kir-heres.*
Context
29“Tumesikia juu ya kiburi cha Moabu:
kutakabari kwake kwa kiburi na majivuno,
kiburi chake na ufidhuli wake,
na kujivuna kwa moyo wake. 30Ninaujua ujeuri wake, lakini ni bure,”
asema Bwana,
“nako kujisifu kwake hakumsaidii chochote. 31Kwa hiyo namlilia Moabu,
kwa ajili ya Moabu yote ninalia,
ninaomboleza kwa ajili
ya watu wa Kir-Haresethi. 32Ninalia machozi kwa ajili yenu, kama Yazeri aliavyo,
enyi mizabibu ya Sibma.
Matawi yako yameenea hadi baharini;
yamefika hadi bahari ya Yazeri.
Mharabu ameyaangukia matunda yako yaliyoiva
na mizabibu yako iliyoiva. 33Shangwe na furaha vimetoweka
kutoka bustani na mashamba ya Moabu.
Nimekomesha kutiririka kwa divai kutoka mashinikizo;
hakuna hata mmoja ayakanyagaye kwa kelele za shangwe.
Ingawa kuna kelele,
sio kelele za shangwe.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.