Yeremia 48:29
Jeremiah 48:29 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Tumesikia juu ya kiburi cha Moabu: kutakabari kwake kwa kiburi na majivuno, kiburi chake na ufidhuli wake, na kujivuna kwa moyo wake.
Jeremiah 48:29 in English
Jeremiah 48:29 · Berean Standard Bible
We have heard of Moab’s pomposity, his exceeding pride and conceit, his proud arrogance and haughtiness of heart.
Context
27Je, Israeli hakuwa kitu chako cha kudhihakiwa?
Je, alikamatwa miongoni mwa wezi,
kiasi cha kutikisa kichwa chako kwa dharau
kila mara unapozungumza juu yake? 28Ondokeni kwenye miji yenu, mkaishi katikati ya miamba,
enyi mnaoishi Moabu.
Kuweni kama huwa ambaye hutengeneza kiota chake
kwenye mdomo wa pango. 29“Tumesikia juu ya kiburi cha Moabu:
kutakabari kwake kwa kiburi na majivuno,
kiburi chake na ufidhuli wake,
na kujivuna kwa moyo wake. 30Ninaujua ujeuri wake, lakini ni bure,”
asema Bwana,
“nako kujisifu kwake hakumsaidii chochote. 31Kwa hiyo namlilia Moabu,
kwa ajili ya Moabu yote ninalia,
ninaomboleza kwa ajili
ya watu wa Kir-Haresethi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.