Native Bible

Jeremiah 48:30 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Ninaujua ujeuri wake, lakini ni bure,” asema Bwana, “nako kujisifu kwake hakumsaidii chochote.

Jeremiah 48:30 in English

Jeremiah 48:30 · Berean Standard Bible

I know his insolence,” declares the LORD, “but it is futile. His boasting is as empty as his deeds.

Context

28Ondokeni kwenye miji yenu, mkaishi katikati ya miamba, enyi mnaoishi Moabu. Kuweni kama huwa ambaye hutengeneza kiota chake kwenye mdomo wa pango. 29“Tumesikia juu ya kiburi cha Moabu: kutakabari kwake kwa kiburi na majivuno, kiburi chake na ufidhuli wake, na kujivuna kwa moyo wake. 30Ninaujua ujeuri wake, lakini ni bure,” asema Bwana, “nako kujisifu kwake hakumsaidii chochote. 31Kwa hiyo namlilia Moabu, kwa ajili ya Moabu yote ninalia, ninaomboleza kwa ajili ya watu wa Kir-Haresethi. 32Ninalia machozi kwa ajili yenu, kama Yazeri aliavyo, enyi mizabibu ya Sibma. Matawi yako yameenea hadi baharini; yamefika hadi bahari ya Yazeri. Mharabu ameyaangukia matunda yako yaliyoiva na mizabibu yako iliyoiva.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.