Yeremia 46:12
Jeremiah 46:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mataifa yatasikia juu ya aibu yako, kilio chako kitaijaza dunia. Shujaa mmoja atajikwaa juu ya mwingine, nao wataanguka chini pamoja.”
Jeremiah 46:12 in English
Jeremiah 46:12 · Berean Standard Bible
The nations have heard of your shame, and your outcry fills the earth, because warrior stumbles over warrior and both of them have fallen together.”
Context
10Lakini ile siku ni ya Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote,
siku ya kulipiza kisasi,
kisasi juu ya adui zake.
Upanga utakula hata utakapotosheka,
hadi utakapozima kiu yake kwa damu.
Kwa maana Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, atatoa dhabihu
kwenye nchi ya kaskazini, kando ya Mto Frati. 11“Panda hadi Gileadi ukapate zeri,
ee Bikira Binti wa Misri.
Lakini umetumia dawa nyingi bila mafanikio;
huwezi kupona. 12Mataifa yatasikia juu ya aibu yako,
kilio chako kitaijaza dunia.
Shujaa mmoja atajikwaa juu ya mwingine,
nao wataanguka chini pamoja.” 13Huu ndio ujumbe Bwana aliomwambia nabii Yeremia kuhusu kuja kwa Nebukadneza mfalme wa Babeli ili kuishambulia Misri: 14“Tangaza hili katika Misri, nawe ulihubiri katika Migdoli,
hubiri pia katika Memfisi* na Tahpanhesi:*
‘Shikeni nafasi zenu na mwe tayari,
kwa kuwa upanga unawala wale wanaokuzunguka.’
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.