Native Bible

Jeremiah 46:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Tangaza hili katika Misri, nawe ulihubiri katika Migdoli, hubiri pia katika Memfisi* na Tahpanhesi:* ‘Shikeni nafasi zenu na mwe tayari, kwa kuwa upanga unawala wale wanaokuzunguka.’

Jeremiah 46:14 in English

Jeremiah 46:14 · Berean Standard Bible

“Announce it in Egypt, and proclaim it in Migdol; proclaim it in Memphis * and Tahpanhes: ‘Take your positions and prepare yourself, for the sword devours those around you.’

Context

12Mataifa yatasikia juu ya aibu yako, kilio chako kitaijaza dunia. Shujaa mmoja atajikwaa juu ya mwingine, nao wataanguka chini pamoja.” 13Huu ndio ujumbe Bwana aliomwambia nabii Yeremia kuhusu kuja kwa Nebukadneza mfalme wa Babeli ili kuishambulia Misri: 14“Tangaza hili katika Misri, nawe ulihubiri katika Migdoli, hubiri pia katika Memfisi* na Tahpanhesi:* ‘Shikeni nafasi zenu na mwe tayari, kwa kuwa upanga unawala wale wanaokuzunguka.’ 15Kwa nini mashujaa wako wamesombwa na kupelekwa mbali? Hawawezi kusimama, kwa maana Bwana atawasukuma awaangushe chini. 16Watajikwaa mara kwa mara, wataangukiana wao kwa wao. Watasema, ‘Amka, turudi kwa watu wetu na nchi yetu, mbali na upanga wa mtesi.’

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.