Native Bible

Jeremiah 46:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kwa nini mashujaa wako wamesombwa na kupelekwa mbali? Hawawezi kusimama, kwa maana Bwana atawasukuma awaangushe chini.

Jeremiah 46:15 in English

Jeremiah 46:15 · Berean Standard Bible

Why have your warriors been laid low? They cannot stand, for the LORD has thrust them down.

Context

13Huu ndio ujumbe Bwana aliomwambia nabii Yeremia kuhusu kuja kwa Nebukadneza mfalme wa Babeli ili kuishambulia Misri: 14“Tangaza hili katika Misri, nawe ulihubiri katika Migdoli, hubiri pia katika Memfisi* na Tahpanhesi:* ‘Shikeni nafasi zenu na mwe tayari, kwa kuwa upanga unawala wale wanaokuzunguka.’ 15Kwa nini mashujaa wako wamesombwa na kupelekwa mbali? Hawawezi kusimama, kwa maana Bwana atawasukuma awaangushe chini. 16Watajikwaa mara kwa mara, wataangukiana wao kwa wao. Watasema, ‘Amka, turudi kwa watu wetu na nchi yetu, mbali na upanga wa mtesi.’ 17Huko watatangaza, ‘Farao mfalme wa Misri ni makelele tu, amekosa wasaa wake.’

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.