Yeremia 46:17
Jeremiah 46:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Huko watatangaza, ‘Farao mfalme wa Misri ni makelele tu, amekosa wasaa wake.’
Jeremiah 46:17 in English
Jeremiah 46:17 · Berean Standard Bible
There they will cry out: ‘Pharaoh king of Egypt was all noise; he has let the appointed time pass him by.’
Context
15Kwa nini mashujaa wako wamesombwa
na kupelekwa mbali?
Hawawezi kusimama, kwa maana Bwana
atawasukuma awaangushe chini. 16Watajikwaa mara kwa mara,
wataangukiana wao kwa wao.
Watasema, ‘Amka, turudi
kwa watu wetu na nchi yetu,
mbali na upanga wa mtesi.’ 17Huko watatangaza,
‘Farao mfalme wa Misri ni makelele tu,
amekosa wasaa wake.’ 18“Kwa hakika kama niishivyo,” asema Mfalme,
ambaye jina lake ni Bwana Mwenye Nguvu Zote,
“mmoja atakuja ambaye ni kama Tabori miongoni mwa milima,
kama Karmeli kando ya bahari. 19Funga mizigo yako kwenda uhamishoni,
wewe ukaaye Misri,
kwa kuwa Memfisi utaangamizwa
na kuwa magofu pasipo mkazi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.