Yeremia 46:11
Jeremiah 46:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Panda hadi Gileadi ukapate zeri, ee Bikira Binti wa Misri. Lakini umetumia dawa nyingi bila mafanikio; huwezi kupona.
Jeremiah 46:11 in English
Jeremiah 46:11 · Berean Standard Bible
Go up to Gilead for balm, O Virgin Daughter of Egypt! In vain you try many remedies, but for you there is no healing.
Context
9Songeni mbele, enyi farasi!
Endesheni kwa ukali, enyi magari ya farasi,
Endeleeni mbele, enyi mashujaa:
watu wa Kushi* na Putu* wachukuao ngao,
watu wa Ludi* wavutao upinde. 10Lakini ile siku ni ya Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote,
siku ya kulipiza kisasi,
kisasi juu ya adui zake.
Upanga utakula hata utakapotosheka,
hadi utakapozima kiu yake kwa damu.
Kwa maana Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, atatoa dhabihu
kwenye nchi ya kaskazini, kando ya Mto Frati. 11“Panda hadi Gileadi ukapate zeri,
ee Bikira Binti wa Misri.
Lakini umetumia dawa nyingi bila mafanikio;
huwezi kupona. 12Mataifa yatasikia juu ya aibu yako,
kilio chako kitaijaza dunia.
Shujaa mmoja atajikwaa juu ya mwingine,
nao wataanguka chini pamoja.” 13Huu ndio ujumbe Bwana aliomwambia nabii Yeremia kuhusu kuja kwa Nebukadneza mfalme wa Babeli ili kuishambulia Misri:
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.