Yeremia 4:9
Jeremiah 4:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Katika siku ile,” asema Bwana “mfalme na maafisa watakata tamaa, makuhani watafadhaika, na manabii watashangazwa mno.”
Jeremiah 4:9 in English
Jeremiah 4:9 · Berean Standard Bible
“In that day,” declares the LORD, “the king and officials will lose their courage. The priests will tremble in fear, and the prophets will be astounded.”
Context
7Simba ametoka nje ya pango lake,
mharabu wa mataifa amejipanga.
Ametoka mahali pake
ili aangamize nchi yenu.
Miji yenu itakuwa magofu
pasipo mtu wa kuishi humo. 8Hivyo vaeni nguo za magunia,
ombolezeni na kulia kwa huzuni,
kwa kuwa hasira kali ya Bwana
haijaondolewa kwetu. 9“Katika siku ile,” asema Bwana
“mfalme na maafisa watakata tamaa,
makuhani watafadhaika,
na manabii watashangazwa mno.” 10Ndipo niliposema, “Aa, Bwana Mwenyezi, umewadanganyaje kabisa watu hawa na Yerusalemu kwa kusema, ‘Mtakuwa na amani,’ wakati upanga uko kwenye koo zetu!” 11Wakati huo watu hawa na Yerusalemu wataambiwa, “Upepo wa moto kutoka miinuko iliyo kame katika jangwa unavuma kuelekea watu wangu, lakini sio kupepeta au kutakasa,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.