Yeremia 4:11
Jeremiah 4:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wakati huo watu hawa na Yerusalemu wataambiwa, “Upepo wa moto kutoka miinuko iliyo kame katika jangwa unavuma kuelekea watu wangu, lakini sio kupepeta au kutakasa,
Jeremiah 4:11 in English
Jeremiah 4:11 · Berean Standard Bible
At that time it will be said to this people and to Jerusalem, “A searing wind from the barren heights in the desert blows toward the daughter of My people, but not to winnow or to sift;
Context
9“Katika siku ile,” asema Bwana
“mfalme na maafisa watakata tamaa,
makuhani watafadhaika,
na manabii watashangazwa mno.” 10Ndipo niliposema, “Aa, Bwana Mwenyezi, umewadanganyaje kabisa watu hawa na Yerusalemu kwa kusema, ‘Mtakuwa na amani,’ wakati upanga uko kwenye koo zetu!” 11Wakati huo watu hawa na Yerusalemu wataambiwa, “Upepo wa moto kutoka miinuko iliyo kame katika jangwa unavuma kuelekea watu wangu, lakini sio kupepeta au kutakasa, 12upepo wenye nguvu sana kuliko wa kupepeta na kutakasa utakuja kwa amri yangu. Sasa natangaza hukumu zangu dhidi yao.” 13Tazama! Anakuja kama mawingu,
magari yake yanakuja kama upepo wa kisulisuli,
farasi wake wana mbio kuliko tai.
Ole wetu! Tunaangamia!
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.