Yeremia 4:12
Jeremiah 4:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
upepo wenye nguvu sana kuliko wa kupepeta na kutakasa utakuja kwa amri yangu. Sasa natangaza hukumu zangu dhidi yao.”
Jeremiah 4:12 in English
Jeremiah 4:12 · Berean Standard Bible
a wind too strong for that comes from Me. Now I also pronounce judgments against them.”
Context
10Ndipo niliposema, “Aa, Bwana Mwenyezi, umewadanganyaje kabisa watu hawa na Yerusalemu kwa kusema, ‘Mtakuwa na amani,’ wakati upanga uko kwenye koo zetu!” 11Wakati huo watu hawa na Yerusalemu wataambiwa, “Upepo wa moto kutoka miinuko iliyo kame katika jangwa unavuma kuelekea watu wangu, lakini sio kupepeta au kutakasa, 12upepo wenye nguvu sana kuliko wa kupepeta na kutakasa utakuja kwa amri yangu. Sasa natangaza hukumu zangu dhidi yao.” 13Tazama! Anakuja kama mawingu,
magari yake yanakuja kama upepo wa kisulisuli,
farasi wake wana mbio kuliko tai.
Ole wetu! Tunaangamia! 14Ee Yerusalemu, usafishe uovu kutoka moyoni mwako na uokolewe.
Utaendelea kuficha mawazo mapotovu mpaka lini?
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.