Native Bible

Jeremiah 4:23 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Niliitazama dunia, nayo haikuwa na umbo tena ni tupu; niliziangalia mbingu, mianga ilikuwa imetoweka.

Jeremiah 4:23 in English

Jeremiah 4:23 · Berean Standard Bible

I looked at the earth, and it was formless and void; I looked to the heavens, and they had no light.

Context

21Hata lini nitaendelea kuona bendera ya vita na kusikia sauti za tarumbeta? 22“Watu wangu ni wapumbavu, hawanijui mimi. Ni watoto wasio na akili, hawana ufahamu. Ni hodari kutenda mabaya, hawajui kutenda yaliyo mema.” 23Niliitazama dunia, nayo haikuwa na umbo tena ni tupu; niliziangalia mbingu, mianga ilikuwa imetoweka. 24Niliitazama milima, nayo ilikuwa ikitetemeka, vilima vyote vilikuwa vikiyumbayumba. 25Nilitazama, wala watu hawakuwepo; kila ndege wa angani alikuwa ameruka zake.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.