Native Bible

Jeremiah 4:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Hata lini nitaendelea kuona bendera ya vita na kusikia sauti za tarumbeta?

Jeremiah 4:21 in English

Jeremiah 4:21 · Berean Standard Bible

How long must I see the signal flag and hear the sound of the horn?

Context

19Ee mtima wangu, mtima wangu! Ninagaagaa kwa maumivu. Ee maumivu makuu ya moyo wangu! Moyo wangu umefadhaika ndani yangu, siwezi kunyamaza. Kwa sababu nimesikia sauti ya tarumbeta, nimesikia kelele ya vita. 20Maafa baada ya maafa, nchi yote imekuwa magofu. Kwa ghafula mahema yangu yameangamizwa, makazi yangu kwa muda mfupi. 21Hata lini nitaendelea kuona bendera ya vita na kusikia sauti za tarumbeta? 22“Watu wangu ni wapumbavu, hawanijui mimi. Ni watoto wasio na akili, hawana ufahamu. Ni hodari kutenda mabaya, hawajui kutenda yaliyo mema.” 23Niliitazama dunia, nayo haikuwa na umbo tena ni tupu; niliziangalia mbingu, mianga ilikuwa imetoweka.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.