Yeremia 29:13
Jeremiah 29:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote.
Jeremiah 29:13 in English
Jeremiah 29:13 · Berean Standard Bible
You will seek Me and find Me when you search for Me with all your heart.
Context
11Kwa maana ninajua mipango niliyo nayo kwa ajili yenu,” asema Bwana, “ni mipango ya kuwafanikisha na wala si ya kuwadhuru, ni mipango ya kuwapa tumaini katika siku zijazo. 12Kisha mtaniita, na mtakuja na kuniomba, nami nitawasikiliza. 13Mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote. 14Nitaonekana kwenu,” asema Bwana, “nami nitawarudisha watu wenu waliotekwa. Nitawakusanya kutoka mataifa yote na mahali pote nilipokuwa nimewafukuzia, nami nitawarudisha mahali ambapo nilikuwa nimewatoa walipochukuliwa uhamishoni,” asema Bwana. 15Mnaweza mkasema, “Bwana ameinua manabii kwa ajili yetu huku Babeli,”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.