Native Bible

Jeremiah 29:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Mnaweza mkasema, “Bwana ameinua manabii kwa ajili yetu huku Babeli,”

Jeremiah 29:15 in English

Jeremiah 29:15 · Berean Standard Bible

Because you may say, “The LORD has raised up for us prophets in Babylon,”

Context

13Mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote. 14Nitaonekana kwenu,” asema Bwana, “nami nitawarudisha watu wenu waliotekwa. Nitawakusanya kutoka mataifa yote na mahali pote nilipokuwa nimewafukuzia, nami nitawarudisha mahali ambapo nilikuwa nimewatoa walipochukuliwa uhamishoni,” asema Bwana. 15Mnaweza mkasema, “Bwana ameinua manabii kwa ajili yetu huku Babeli,” 16lakini hili ndilo asemalo Bwana kuhusu mfalme aketiaye kiti cha enzi cha Daudi, na watu wa kwenu wote wanaobaki katika mji huu, ndugu zenu ambao hawakwenda pamoja nanyi uhamishoni. 17Naam, hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote: “Nitatuma upanga, njaa na tauni dhidi yao, nami nitawafanya kuwa kama tini dhaifu zile ambazo ni mbovu sana zisizofaa kuliwa.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.