Yeremia 29:14
Jeremiah 29:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nitaonekana kwenu,” asema Bwana, “nami nitawarudisha watu wenu waliotekwa. Nitawakusanya kutoka mataifa yote na mahali pote nilipokuwa nimewafukuzia, nami nitawarudisha mahali ambapo nilikuwa nimewatoa walipochukuliwa uhamishoni,” asema Bwana.
Jeremiah 29:14 in English
Jeremiah 29:14 · Berean Standard Bible
I will be found by you, declares the LORD, and I will restore you from captivity * and gather you from all the nations and places to which I have banished you, declares the LORD. I will restore you to the place from which I sent you into exile.”
Context
12Kisha mtaniita, na mtakuja na kuniomba, nami nitawasikiliza. 13Mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote. 14Nitaonekana kwenu,” asema Bwana, “nami nitawarudisha watu wenu waliotekwa. Nitawakusanya kutoka mataifa yote na mahali pote nilipokuwa nimewafukuzia, nami nitawarudisha mahali ambapo nilikuwa nimewatoa walipochukuliwa uhamishoni,” asema Bwana. 15Mnaweza mkasema, “Bwana ameinua manabii kwa ajili yetu huku Babeli,” 16lakini hili ndilo asemalo Bwana kuhusu mfalme aketiaye kiti cha enzi cha Daudi, na watu wa kwenu wote wanaobaki katika mji huu, ndugu zenu ambao hawakwenda pamoja nanyi uhamishoni.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.