Yeremia 22:9
Jeremiah 22:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nalo jibu litakuwa: ‘Kwa sababu wameliacha agano la Bwana, Mungu wao, na wameabudu na kuitumikia miungu mingine.’ ”
Jeremiah 22:9 in English
Jeremiah 22:9 · Berean Standard Bible
Then people will reply, ‘Because they have forsaken the covenant of the LORD their God and have worshiped and served other gods.’”
Context
7Nitawatuma waharabu dhidi yako,
kila mtu akiwa na silaha zake,
nao watazikata boriti zako nzuri za mierezi
na kuzitupa motoni. 8“Watu kutoka mataifa mengi watapitia karibu na mji huu na kuulizana, ‘Kwa nini Bwana amefanya jambo la namna hii juu ya mji huu mkubwa?’ 9Nalo jibu litakuwa: ‘Kwa sababu wameliacha agano la Bwana, Mungu wao, na wameabudu na kuitumikia miungu mingine.’ ” 10Usimlilie yeye aliyekufa, wala usimwombolezee;
badala yake, afadhali umlilie kwa uchungu
yule aliyepelekwa uhamishoni,
kwa sababu kamwe hatairudia
wala kuiona tena nchi yake alikozaliwa. 11Kwa kuwa hili ndilo asemalo Bwana kuhusu Shalumu* mwana wa Yosia, aliyeingia mahali pa baba yake kuwa mfalme wa Yuda, lakini ameondoka mahali hapa: “Yeye kamwe hatarudi tena.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.