Yeremia 22:10
Jeremiah 22:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Usimlilie yeye aliyekufa, wala usimwombolezee; badala yake, afadhali umlilie kwa uchungu yule aliyepelekwa uhamishoni, kwa sababu kamwe hatairudia wala kuiona tena nchi yake alikozaliwa.
Jeremiah 22:10 in English
Jeremiah 22:10 · Berean Standard Bible
Do not weep for the dead king; do not mourn his loss. Weep bitterly for the one who is exiled, for he will never return to see his native land.
Context
8“Watu kutoka mataifa mengi watapitia karibu na mji huu na kuulizana, ‘Kwa nini Bwana amefanya jambo la namna hii juu ya mji huu mkubwa?’ 9Nalo jibu litakuwa: ‘Kwa sababu wameliacha agano la Bwana, Mungu wao, na wameabudu na kuitumikia miungu mingine.’ ” 10Usimlilie yeye aliyekufa, wala usimwombolezee;
badala yake, afadhali umlilie kwa uchungu
yule aliyepelekwa uhamishoni,
kwa sababu kamwe hatairudia
wala kuiona tena nchi yake alikozaliwa. 11Kwa kuwa hili ndilo asemalo Bwana kuhusu Shalumu* mwana wa Yosia, aliyeingia mahali pa baba yake kuwa mfalme wa Yuda, lakini ameondoka mahali hapa: “Yeye kamwe hatarudi tena. 12Atafia huko mahali walipompeleka kuwa mateka; hataiona tena nchi hii.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.