Native Bible

Jeremiah 22:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Watu kutoka mataifa mengi watapitia karibu na mji huu na kuulizana, ‘Kwa nini Bwana amefanya jambo la namna hii juu ya mji huu mkubwa?’

Jeremiah 22:8 in English

Jeremiah 22:8 · Berean Standard Bible

And many nations will pass by this city and ask one another, ‘Why has the LORD done such a thing to this great city?’

Context

6Kwa kuwa hili ndilo Bwana asemalo kuhusu jumba la kifalme la mfalme wa Yuda: “Ingawa uko kama Gileadi kwangu, kama kilele cha Lebanoni, hakika nitakufanya uwe kama jangwa, kama miji ambayo haijakaliwa na watu. 7Nitawatuma waharabu dhidi yako, kila mtu akiwa na silaha zake, nao watazikata boriti zako nzuri za mierezi na kuzitupa motoni. 8“Watu kutoka mataifa mengi watapitia karibu na mji huu na kuulizana, ‘Kwa nini Bwana amefanya jambo la namna hii juu ya mji huu mkubwa?’ 9Nalo jibu litakuwa: ‘Kwa sababu wameliacha agano la Bwana, Mungu wao, na wameabudu na kuitumikia miungu mingine.’ ” 10Usimlilie yeye aliyekufa, wala usimwombolezee; badala yake, afadhali umlilie kwa uchungu yule aliyepelekwa uhamishoni, kwa sababu kamwe hatairudia wala kuiona tena nchi yake alikozaliwa.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.