Yeremia 22:12
Jeremiah 22:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Atafia huko mahali walipompeleka kuwa mateka; hataiona tena nchi hii.”
Jeremiah 22:12 in English
Jeremiah 22:12 · Berean Standard Bible
but he will die in the place to which he was exiled; he will never see this land again.”
Context
10Usimlilie yeye aliyekufa, wala usimwombolezee;
badala yake, afadhali umlilie kwa uchungu
yule aliyepelekwa uhamishoni,
kwa sababu kamwe hatairudia
wala kuiona tena nchi yake alikozaliwa. 11Kwa kuwa hili ndilo asemalo Bwana kuhusu Shalumu* mwana wa Yosia, aliyeingia mahali pa baba yake kuwa mfalme wa Yuda, lakini ameondoka mahali hapa: “Yeye kamwe hatarudi tena. 12Atafia huko mahali walipompeleka kuwa mateka; hataiona tena nchi hii.” 13“Ole wake yeye ajengaye jumba lake la kifalme kwa njia ya dhuluma,
vyumba vyake vya juu kwa udhalimu,
akiwatumikisha watu wa nchi yake pasipo malipo,
bila kuwalipa kwa utumishi wao. 14Asema, ‘Nitajijengea jumba kuu la kifalme,
na vyumba vya juu vyenye nafasi kubwa.’
Hivyo anaweka ndani yake madirisha makubwa,
huweka kuta za mbao za mierezi,
na kuipamba kwa rangi nyekundu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.