Yeremia 22:19
Jeremiah 22:19 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Atazikwa maziko ya punda: ataburutwa na kutupwa nje ya malango ya Yerusalemu.”
Jeremiah 22:19 in English
Jeremiah 22:19 · Berean Standard Bible
He will be buried like a donkey, dragged away and thrown outside the gates of Jerusalem.
Context
17“Lakini macho yako na moyo wako vimeelekezwa tu
katika mapato ya udhalimu,
kwa kumwaga damu isiyo na hatia,
kwa uonevu na ukatili.” 18Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana kuhusu Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda:
“Hawatamwombolezea wakisema:
‘Ole, ndugu yangu! Ole, umbu langu!’
Hawatamwombolezea wakisema:
‘Ole, bwana wangu! Ole, fahari yake!’ 19Atazikwa maziko ya punda:
ataburutwa na kutupwa
nje ya malango ya Yerusalemu.” 20“Panda Lebanoni ukapige kelele,
sauti yako na isikike huko Bashani,
piga kelele toka Abarimu,
kwa kuwa wote waliojiunga nawe wameangamizwa. 21Nilikuonya wakati ulipojisikia kwamba uko salama,
lakini ulisema, ‘Mimi sitasikiliza!’
Hii imekuwa kawaida yako tangu ujana wako;
hujanitii mimi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.