Native Bible

Jeremiah 22:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Nilikuonya wakati ulipojisikia kwamba uko salama, lakini ulisema, ‘Mimi sitasikiliza!’ Hii imekuwa kawaida yako tangu ujana wako; hujanitii mimi.

Jeremiah 22:21 in English

Jeremiah 22:21 · Berean Standard Bible

I warned you when you were secure. You said, ‘I will not listen.’ This has been your way from youth, that you have not obeyed My voice.

Context

19Atazikwa maziko ya punda: ataburutwa na kutupwa nje ya malango ya Yerusalemu.” 20“Panda Lebanoni ukapige kelele, sauti yako na isikike huko Bashani, piga kelele toka Abarimu, kwa kuwa wote waliojiunga nawe wameangamizwa. 21Nilikuonya wakati ulipojisikia kwamba uko salama, lakini ulisema, ‘Mimi sitasikiliza!’ Hii imekuwa kawaida yako tangu ujana wako; hujanitii mimi. 22Upepo utawaondoa wachungaji wako wote, na wale ulioungana nao wataenda uhamishoni. Kisha utaaibika na kufedheheka kwa sababu ya uovu wako wote. 23Wewe uishiye Lebanoni, wewe uliyetulia kwenye majengo ya mierezi, tazama jinsi utakavyoomboleza maumivu makali yatakapokupata, maumivu kama yale ya mwanamke mwenye utungu wa kuzaa!

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.